Skip to main content

Posts

MKUTANO MKUU WA 13 WA VIJANA TAIFA 2022

Mkutano mkuu wa vijana wa Kanisa la Wabaptist  Tanzania. Mkutano wa 13 wa mwaka 2022 wa Idara ya Vijana Kanisa la Wabaptist Tanzania unatarajiwa kufanyika iringa tarehe 23-26 Juni 2022. Vjana wote wanashauriwa kuwasiliana na Viongozi wao wa Majimbo na Kanda kwa ajili ya kupata taarifa ndani kuhusiana na Mkutano huo.  Aidha mnajulishwa kuwa Juma la Vijana kitaifa kwa mwaka huu litafanyikia Sumbawanga Juma la mwisho la mwezi wa Mei 2022.   Kwa taarifa za mikutano mingine na matukio ya Vijana wa Kanisa la Wabaptist Tanzania tembelea tovuti yetu.  Imetolewa na Idara ya Vijana Kanisa la Wabaptist Tanzania

MKUTANO MKUU WA KANISA LA WABAPTIST MWAKA 2022

Baptists' Church of Tanzania  Annual General Meeting 2022 Date 5-8 July, 2022 « TUNA NGUVU KULIKO MWANZO                               MKUTANO MKUU WA KANISA LA WABAPTIST  TANZANIA TAREHE 5-8 JULAI  MWAKA 2022 Coming soon! MKUTANO UNAFANYIKIA JIJINI DODOMA  Kiingilio kila kanisa 100,000/=  Kila mjumbe 60,000/= HUU NI MKUTANO WA 46  WA KANISA, UTAKAOSHUHUDIWA NA MAMIA YA WAJUMBE KUTOKA MAKANISANI. KILA KANISA LINATARAJIWA KUTUMA WAJUMBE WATATU.  MKUTANO HUU UTAKUWA NI WA UCHGUZI MKUU WA VIONGOZI WA KANISA NGZI YA TAIFA   For more details call General Secretary office at +255787118575   

WABAPTIST WALIFANYA MAAMUZI MBEYA MWAKA 2015

 Viongozi wakuu wastaafu wa Jumuiya Kuu ya Wabaptist wa Tnzania Kushoto ni Mwenyekiti Mstaafu wa taifa Mch Harry Mwasanjala, anaefuata ni Rev Arnold Manase Mwenyekiti wa Jumuiya Kuu wa sasa, wa tatu ni Rev Dr Edward Mwaijande mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya Kuu, na kulia ni Kiongozi mstaafu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mch A. Maboko wakiwa kweye picha ya pamoja mara baada ya kupitisha katiba mjini Mbeya. Mkutano wa mwaka uliohudhuriwa na zaidi ya wajumbe 230 kutoka nchi nzima.  Wachungaji toka kila mkoa wakiinua mikono yao, huku wakifuatilia na kukubaliana kwa pamoja kwenye mkutano wa mwaka.  Zilikuwa siku tatu za bunge la Wabaptist wa Tanzania za kuchambua rasimu ya katiba kifungu hadi kifungu.  Rev Kelly Zeramula akiwaongoza wachungaji maombi picha ya chini ni Mzee Patrick Sombe  Mwenyekiti wa Halmshauri ya Chuo Kikuu cha Mount Meru University akishiriki mkutano mkuu.  Rev Mch Arnold Manase akifunga mkutano wa katiba hapa chuo cha TE...

Current Leaders

BAPTISTS' CHURCH OF TANZANIA  CURRENT LEADERS: Executive Office Bearers:               1. Rev Arnold Manase Mollel     - General Overseer of Baptists' Church  of Tanzania                           2. Rev Dickson A. Mwankanda       - Vice General Overseer  of Baptists' Church of Tanzania                 3. Rev Michael Peter Nhonya        - General Secretary of Baptists' Church of Tanzania                4. Rev Amri Msabila Kihumbi     - Assistant Secretary of Baptist's Church of Tanzania   5. Mrs Atupele Banda Kyando       - Treasurer of Baptists' Church  of Tanzani    6. Mr. Simon Runda Marivey      -Assistant Treasurer of Baptists' of Tanzania ...

Picha na matukio wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Vijana Taifa Iringa

                Mwenyekiti BCT Mchungaji A. Manase akihubiri Injili wakati wa ufunguzi wa mkutano wa vijana Iringa                  Chini kwenye picha na Mwenyekiti wa vijana Taifa Bw Julius Mkapa akifuatilia

HOTUBA YA UFUNGUZI MKUTANO MKUU VIJANA WA BAPTIST TANZANIA 2015

TUMEITWA KUTUMIKA Hii ni kauli mbiu ya mwaka 2015 kwa vijana wa Kanisa la Baptist Tanzania. Mwenyekiti wa makanisa ya Kibaptist Tanzania Mch Arnold Manase, alifungua mkutano huo leo tarehe 2 July, 2015 majira ya saa 7:01 akiongea kwa takribani saa nzima amewaasa na kuwakumbusha vijana wa Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania kwamba WAMEITWA KUTUMIKA , amesema hii ni karne ya kujenga kanisa lenye nguvu na lenye waumini wengi. Hii ndio dira ya dhehebu kwa mwaka 2015-2020. Na kwamba ili uwe na kanisa lenye nguvu na lenye waumini wengi lazima  1.        Uwe na nguvu ya uchumi 2.        Uwe na watenda kazi imara 3.        Vjana wamjuao Mungu 4.        Vijana wanaotembea na Mungu 5.        Vijanawanaoweza kuishawishi Jamii na kuiletea mabadiliko 6.        Na Uwe na vijana wawajibikaji Akisoma k...

Picha za Viongozi na Matukio

 Mwangalizi  wa Jumuiya Kuu Wabaptist wa TZ Rev Arnold Manase akiwa na Mhubiri wa Kimataifa Mjukuu wa Bill Graham, Rev Dr Will F. Graham kutoka Marekani alipokuja kuhubiri Arusha na Kukutana na Wabaptist wa Arusha tarehe 26 June 2015.  Baadhi ya Wachungaji wa Kanda ya Kaskazini wakiwa kwenye picha ya pamoja na Dr Will Graham  Picha chini ni baadhi ya wanawake wakimpatia zawadi Dr Graham kwa niaba ya Idara ya wanawake BCT