TUMEITWA KUTUMIKA
Hii ni kauli mbiu ya mwaka 2015 kwa vijana wa Kanisa la
Baptist Tanzania. Mwenyekiti wa makanisa ya Kibaptist Tanzania Mch Arnold
Manase, alifungua mkutano huo leo tarehe 2 July, 2015 majira ya saa 7:01
akiongea kwa takribani saa nzima amewaasa na kuwakumbusha vijana wa Jumuiya Kuu
ya Wabaptist Tanzania kwamba WAMEITWA KUTUMIKA, amesema hii ni karne ya kujenga kanisa lenye nguvu na lenye waumini wengi. Hii ndio dira ya dhehebu kwa mwaka
2015-2020. Na kwamba ili uwe na kanisa lenye nguvu na lenye waumini wengi
lazima
1.
Uwe na nguvu ya uchumi
2.
Uwe na watenda kazi imara
3.
Vjana wamjuao Mungu
4.
Vijana wanaotembea na Mungu
5.
Vijanawanaoweza kuishawishi Jamii na kuiletea
mabadiliko
6.
Na Uwe na vijana wawajibikaji
Akisoma kitabu cha Daniel 1:3-6 “Mfalme akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matowashi wake, awalete
baadhi ya wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa kiungwana; 4vijana
wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa
yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena
alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao. 5Huyo mfalme
akawaagizia posho ya chakula cha mfalme, na ya divai aliyokunywa, akaagiza
walishwe hivyo muda wa miaka mitatu; ili kwamba hatimaye wasimame mbele ya
mfalme.
6 Basi katika hao walikuwapo baadhi
ya wana wa Yuda, Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria. 7Mkuu wa
matowashi akawapa majina; alimwita Danieli, Belteshaza; na Hanania akamwita
Shadraka; na Mishaeli akamwita Meshaki; na Azaria akamwita Abednego.”
Comments
Post a Comment