Kanisa la Wabaptist Tanzania linawatakia Watanzania wote na marafiki zetu mlioko popote duniani kila la kheri mnapomaliza mwaka 2021 na kuingia mwaka 2022. Tuunawapongeza wote mliosimamia imani yenu katika Bwana kwa kipindi chote cha mapito ambayo knisa limepitia na Watanzania na watu wote ulimwengu kama mjuavyo kuwa janga la UVIKO 19 limeu watu wengi na kufanya uchumi kudolola katika baadhi ya mataifa.
Hivyo basi tutumie sikukuu hizi kumshukuru Mungu kwa Rehema zake na kwa kupa sisi tulio hai leo nafasi nyingine. Tukumbyke kuwa kila kunapopamabazuka ni fursa nyingine tupewayo na Mungu na tujiulize sana Mungu ametupatia nafsi nyingine ili iweje.
Bila shaka tutebnde mapenzi yake na tumtumikie kwa bidii zaidi.
Ahsanteni sana tunawatakia kila la kheri
AMANI NA UPENDO UDUMU!
Rev Michael Peter Nhonya
KATIBU MKUU
KANISA LA WABAPTIST TANZANIA
Comments
Post a Comment