Skip to main content

Posts

MKITANO MKUU WA 46 DODOMA

 Mkutano Mkuu wa 46 Kanisa la wabaptist Tanzania kufanyika tarehe 27-29 Julai 2022 Dodoma jiji.  Wajumbe wote wa Mkutano mkuu watawasili Dodoma tarehe 27 Julai 2022 jioni. Tafadhali pata maelekezo kwa viongozi wako wa kanda kwa taarifa zaidi. 
Recent posts

PICHA NA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA

  Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Prof Palamagamba Kabudi Mwaluko katika Hafla ya Usimikaji Viongozi wa Kanda PWANI & KATI Jijini Dar es Salaam (wa tatu katika kati) 

Salaam za Krisms na Mwaka Mpya 2022

Kanisa la Wabaptist Tanzania linawatakia Watanzania wote na marafiki zetu mlioko popote duniani kila la kheri mnapomaliza mwaka 2021 na kuingia mwaka 2022. Tuunawapongeza wote mliosimamia imani yenu katika Bwana kwa kipindi chote cha mapito ambayo knisa limepitia na Watanzania na watu wote ulimwengu kama mjuavyo kuwa janga la UVIKO 19 limeu watu wengi na kufanya uchumi kudolola katika baadhi ya mataifa.  Hivyo basi tutumie sikukuu hizi kumshukuru Mungu kwa Rehema zake na kwa kupa sisi tulio hai leo nafasi nyingine. Tukumbyke kuwa kila kunapopamabazuka ni fursa nyingine tupewayo na Mungu na tujiulize sana Mungu ametupatia nafsi nyingine ili iweje.  Bila shaka tutebnde mapenzi yake na tumtumikie kwa bidii zaidi.  Ahsanteni sana tunawatakia kila la kheri  AMANI NA UPENDO UDUMU! Rev Michael Peter Nhonya KATIBU MKUU KANISA LA WABAPTIST TANZANIA

Viongozi Wakuu Kanisa la Baptist Tanzania Wakiwa Ikulu na Makamu wa Rais wa Tanzania

Dr Philipo Isidory Mpango Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akutana na Viongozi Wakuu wa Kanisa la Wabaptist Tanzania Ikulu Chamwino Jijini Dodoma. Viongozi hawa walipata fursa kuzungumzi mswala mbalimbali ya Nchi na Ustawi wa Taifa la Tanzania.   

Picha na Matukio Mkutano Mkuu wa Wabaptist Tanzania 2020 Jijini Arusha

  DIRA YA UONGOZI HUU WA AWAMU YA 10 CHINI YA MWANGALIZI MKUU REV ARNOLD MANASE  NI: “KUJENGA KANISA LENYE NGUVU KIROHO, KIIDADI, NA KIUCHUMI.”